Twitter | Search | |
millardayo
117,855
Tweets
590
Following
832,786
Followers
Tweets
millardayo 2h
Leo hii wajanja wote wanaangalia movie kwenye app ya . Fanya kupakua app uweze kufurahia movie na tamthilia popote ulipo!
Reply Retweet Like
millardayo 4h
TCRA imepiga marufuku Watu wenye vitambulisho vya NIDA kuwasajilia wenzao wasiokuwa navyo laini zao kwa alama za vidole “atakayebainika anamsajilia mwenzake adhabu ni kulipa faini isiyopungua Million 5 au kwenda jela miezi sita au adhabu zote kwa pamoja”
Reply Retweet Like
millardayo 5h
Abiria wanaosafiri kutoka DSM kwenda Mikoa ya Kusini wamekwama maeneo ya Mlima wa Mbagala Kokoto DSM baada ya Lori kushindwa kupanda Mlima na kuharibika katikati ya Barabara na kusababisha foleni kubwa tangu saa kumi na mbili asubuhi hadi muda huu
Reply Retweet Like
millardayo 6h
Dangote (62) ni Tajiri namba moja Afrika akiwa na USD Billion 10.1, Nassef Sawiris (58) mwenye USD Billion 08 yupo nafasi ya pili,na No. 3 ni Mike Adenuga(66) USD Billion 7.7, katika Nchi zote za Afrika ni Nchi 8 pekee zenye Mabilionea huku Tanzania ikijivunia kuwa na Mo Dewji.
Reply Retweet Like
millardayo 6h
Katika ripoti yake mpya Forbes imesema Mfanyabiashara wa Nigeria Aliko Dangote ameendelea kuwa Bilionea No.1 Afrika akiwa na utajiri wa USD Billion 10.1 ( Trilion 23.31 za Kitanzania) licha ya kwamba na yeye utajiri wake umepungua kutoka Billion 10.3 (Trilion 23.78) mwaka jana.
Reply Retweet Like
millardayo 6h
Mo Dewji licha ya kupoteza USD Million 300 (Billion 692.67) na kuwa na utajiri wa USD Billion 1.6 (Trilion 3.69) ukilinganisha na tathmini ya mwaka jana ambapo alikuwa na USD Billion 1.9 (Trilion 4.3), ameendelea kubaki No.1 kwenye orodha ya Mabilionea wenye umri mdogo Afrika.
Reply Retweet Like
millardayo 7h
Mfanyabiashara Mo Dewji ametajwa tena na ripoti mpya ya jarida la Forbes kuwa ni Mfanyabiashara tajiri mdogo kuliko wote Afrika kwa mwaka wa sita mfululizo akikadiriwa kuwa na utajiri wa Dola za Kimarekani Billion 1.6 (Trilion 3.69 za Kitanzania)
Reply Retweet Like
millardayo 7h
Uzoefu wa miaka kwenye kusafirisha mizigo kutoka China kuja Afrika, NAMBA MOJA wa wakati wote ni Silent_ocean_ltd ✊🏿
Reply Retweet Like
millardayo 9h
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo January 18,2020
Reply Retweet Like
millardayo 15h
Club ya Inter Milan ya Italia imemsajili aliyekuwa nahodha wa Man United Ashley Young (34) kwa mkataba wa miezi sita hadi mwisho wa msimu, Inter Milan wamemnunua kwa pound milioni 1.5 (Tsh Bilioni 4.4)
Reply Retweet Like
millardayo 19h
“Nafurahi sana kumkaribisha RC wetu, Mnyama mwenzangu Paul Makonda kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya Simba akiwa kama Mshauri Mkuu (Senior Advisor), Karibu kaka, pamoja tutajenga Simba bora zaidi! hongera kwa uteuzi“ - MO DEWJI
Reply Retweet Like
millardayo 21h
Kufuatia madai ya Raia wa kigeni kunyimwa chakula Keko na kupelekea Raia wa Burundi Habonimana Nyandwi ambaye ni mshitakiwa ktk kesi ya mauaji ya Wayne Lotter kuzimia Mahakamani kisa njaa, Hakimu Isaya ameahirisha kesi hadi Jan 24,2020 ili kupata taarifa zaidi juu ya malalamiko.
Reply Retweet Like
millardayo 21h
Licha ya Askari Magereza kuiambia Mahakama ya Kisutu kuwa Mahabusu wote wanapata chakula,Mshtakiwa Ayubu amedai ktk Mahabusu ya Keko Raia wa Kigeni ni wengi na wote wanapata chakula kwa wakati, isipokuwa Watuhumiwa wawili wa Mauaji ya Lotter ambao wamekatiwa huduma kwa siku tano.
Reply Retweet Like
millardayo 21h
Baada ya Nyandwi kuzimia kisa njaa, mwenzie Zebadayo ameangua kilio kwa nguvu Mahakama ya Kisutu akidai Raia wa kigeni waliopo ktk kesi ya Mauaji ya Lotter hawajui ushiriki wao na hawana Ndugu wa kuwapa chakula Tanzania “tumedhoofika, Gerezani tunanyimwa chakula leo siku ya tano"
Reply Retweet Like
millardayo 21h
Raia wa Burundi, Habonimana Nyandwi ambaye ni mshitakiwa katika kesi ya mauaji ya Mwanaharakati wa Tembo, Wayne Lotter amezimia katika Mahakama ya Kisutu chanzo kikidaiwa ni njaa, alishindwa kusimama na kudondoka akigeuza macho, Polisi wakamsogelea na kumvua viatu na mkanda.
Reply Retweet Like
millardayo retweeted
millardayo Jan 16
Kuna uwezekano wa asilimia 80 ya Samatta kujiunga na AstonVilla, taarifa za chini ya kapeti zinaeleza kocha wa AstonVilla Dean Smith anamuona Samatta kama mbadala mshambuliaji Wesley aliyeumia goti dau la Samatta linatajwa kuwa pound milioni 10 (Tsh bilioni 30)
Reply Retweet Like
millardayo 23h
Elimu haina mwisho, walisikika wahenga wakisema. wanakuletea Safari ya Gwalu. Movie yenye kufundisha na kufurahisha. Pakua app sasa uburudike na movie pamoja na tamthilia nyingine.
Reply Retweet Like
millardayo 24h
Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo amemuagiza Mkurugenzi wa Dodoma Godwin Kunambi kumuongezea mshahara Esther Nyange ambaye ni Dereva wa gari la kupakulia taka ktk dampo la Jiji la Dodoma ambaye analipwa Tsh.240,000 “Mtoto mzuri,mrembo mnamlipa Laki mbili?”
Reply Retweet Like
millardayo retweeted
millardayo Jan 17
Alejandrina Guzman,Mtoto wa Kike wa muuza unga maarufu Duniani Joaquín "El Chapo" Guzmán anayetumikia kifungo Gerezani, ametangaza kuja na Bia yenye Brand ya Baba yake ‘El Chapo Lager’ kama ishara ya heshima kwa Chapo “Alcohol ni 4%, imetengenezwa kwa nafaka na asali” (@ Reuters)
Reply Retweet Like
millardayo Jan 17
Nchi tano zilizopoteza Raia wake baada ya Iran kuidungua ndege iliyoua Watu 176, Canada,Ukraine,Sweden, Afghanistan na Uingereza zimetoa taarifa ya pamoja ya kuitaka Iran kulipa fidia kwa Familia za wahanga “tunasisitiza Iran lazima ihakikishe pia inafanya uchunguzi huru na wazi”
Reply Retweet Like